Dkt.Diallo awataka wakulima wilayani Ngara kutumia mbolea

KAGERA-Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo amewataka wakulima mkoani Kagera kujikita kwenye kilimo cha kisasa kwa kutumia mbolea ili kuongeza tija ya uzalishaji kwenye mazao mbalimbali shambani.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo akizungumza katika kikao kifupi baina ya wajumbe wa bodi, Menejimenti ya TFRA na wajumbe wa Bodi ya Chama cha Wakulima Ngara kilichofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Ngara.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo akimsikiliza mjumbe wa Bodi ya Chama cha Wakulima cha Ngara, Severian Mtuku akiwasilisha taarifa fupi ya Chama katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Chama wilayani Ngara tarehe 13 Aprili, 2024.

Dkt. Diallo ametoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wakulima na mawakala wa usambazaji wa mbolea za ruzuku wilayani Ngara.

"Nia yetu kubwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi wakulima kwa kuongeza uzalishaji baada ya kutumia mbolea zitakazopelekea kuongeza tija kwenye uzalishaji," Dkt. Diallo alikazia.Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent akizungumza jambo mara baada ya wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya TFRA kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa Chama cha Wakulima Ngara (Ngara Farmers Association Ltd) tarehe 13 Aprili, 2024.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent amewataka wakulima kuwekeza zaidi kwenye kupima afya ya udongo ili waweze kutumia mbolea inayoendana na uhitaji wa udongo.Meneja wa TFRA Kanda ya Ziwa, Michael Sanga akizungumza wakati wa kikao na wajumbe wa Bodi ya Chama cha Wakulima Ngara wilayani Ngara tarehe 13 Aprili, 2024.

Amesema, matumizi sahihi ya mbolea yanaleta tija kwenye uzalishaji hivyo nakuwasihi wakulima kuendelea kutumia mbolea sahihi kulingana na uhitaji wa udongo wao baada ya kuupima.

Naye Kaimu Meneja wa Chama cha Wakulima Ngara, Fadhili Damian Kamhanda amesema Wilaya ya Ngara ilifanikiwa kupokea tani 65 za mbolea sawa na mifuko 1300 iliyosambazwa kwa wakulima kwa asilimia 98.

Amesema, chama chao kiliingia mkataba na kampuni za OCP na Minjingu ili kusambaza mbolea za ruzuku ambapo ni mara ya kwanza kwa mbolea kufikishwa wilayani humo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo akimsikiliza mjumbe wa Bodi ya Chama cha Wakulima cha Ngara, Severian Mtuku akiwasilisha taarifa fupi ya Chama katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Chama wilayani Ngara tarehe 13 Aprili, 2024.

Kwa upande wake Mkulima mnufaika wa mbolea za ruzuku, Fred Gahanga amesema amenufaika na mbolea za ruzuku na anategemea kufanya vizuri kwenye uzalishaji kwa msimu huu wa kilimo.

"Basi mimi nilijaribu tu kutumia mbolea kwenye ekari moja nikaona ni kweli ukitumia mbolea naweza kuvuna kuanzia kilo 30 hadi 35," Fredy amesisitiza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news