Maelfu wampokea Dkt.Mwigulu Nchemba jimboni,atatua changamoto papo kwa hapo

SINGIDA-Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ameendelea na ziara yake ya kupokea na kutatua changamoto papohapo jimboni humo, ambapo siku ya jana amefanya ziara kata za Doromoni, Kidaru na Kisiriri.
Akiwa katika maeneo hayo Dkt.Nchemba amesikiliza changamoto, maoni na kero mbalimbali za wananchi hao na kuzipatia utatuzi papohapo.

Maelfu ya wananchi wa Jimbo hilo wameendelea kumiminika katika ziara hiyo inayoendelea katika viunga mbalimbali vya wilaya ya Iramba.
Dkt.Nchemba ameambatana wa viongozi wenzake mbalimbali wa wilayani humo wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda, Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Iramba na madiwani wa halmashauri hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news