Mheshimiwa Mwassa awauma sikio maafisa tarafa na watendaji wa kata

KAGERA-Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa Fatma Mwassa amewataka maafisa tarafa na watendaji wa kata kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi yake kwa kuwa Serikali inaendelea kusisitiza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato.
Ameyasema hayo Aprili 23, 2024 wakati wa akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa tarafa na watendaji wa kata wa Mkoa wa Kagera yaliyofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Bukoba Sekondari.
Mhe. Mwassa amesema, Serikali inaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi ili kuwajengea uwezo wa kuweza kufanya kazi kwa ubunifu na waledi.

Pia,kuwataka kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na matumizi yake kwa kushirikiana na viongozi wa wananchi na watendaji wengine walipo katika maeneo yao ya kazi waliopo ngazi ya msingi."Bila ushirikiano hakuna mafanikio," Mheshimiwa Mwassa amesema.
Pia, amewasisitiza maafisa hao kufuatilia na kusimamia vizuri fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoletwa na Serikali katika maeneo yao ili fedha hizo zilete matokea tarajiwa na kuwaondolea wananchi changamoto za kukosa huduma.

“Nyie ndio mpo katika kazi za msingi mnapaswa kufahamu na kuzingatia kanuni na maadili na kutumia misingi ya haki badala ya upendeleo pale mnapotoa huduma kwa wananchi na kuweka vizuri malengo halisi ya kazi zenu ili kuwawezesha kufikia kiwango cha juu katika utendaji wenu wa kazi kwa kuwatendea haki wananchi katika utoaji wa huduma,”amesema Mheshimiwa Mwassa.
Aidha, Mhe. Mwassa amewataka maafisa tarafa na watendaji wa kuhakikisha wanasimamia usalama, amani na utulivu vinakuwepo kwenye maeneo yao wakati wote ikizingatiwa suala la usalama ni jukumu la kila mwananchi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama katika maeneo yao.
“Kero ndogo ndio uzaa kubwa kwahiyo tujitahidi sana kutatua hizi kero ndogo ndogo ili tusije kutengeneza vinyongo na chuki kwa wananchi na Serikali yao.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news