Rais Dkt.Mwinyi:Zanzibar itaendelea kuudumisha Muungano daima

DAR ES SALAAM-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Zanzibar itaendelea kuwa muumini wa dhati wa Muungano kwa kuudumisha na kuuimarisha kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Aprili 26,2024 wakati akizungumza katika kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yalioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Imeendelea kupata sifa na heshima kubwa kimataifa kwa kuwa nchi ya mfano kwa kudumu kwa Muungano wa kuwa na amani, umoja na mshikamano.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa yaliyotokana na Muungano katika sekta mbalimbali kiuchumi na huduma za kijamii.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewashukuru Viongozi wa awamu zilizopita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada za kudumisha na kuendeleza malengo ya Tanzania na kuzifanyia kazi changamoto zinazojitokeza na kuzifanyia ufumbuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news