Mwenyekiti wa Kijiji jela kwa kupokea hongo awagawie wanakijiji mashamba

KATAVI-Aprili 12, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi mbele ya Hakimu Mfawidhi, Mheshimiwa Sydney Nindi imefunguliwa kesi ya Jinai namba CC. 9586/2024 ya Jamhuri.
Ni dhidi ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagunga Kata ya Kasekese wilayani humo, Ntunga Sahani Kuwasanya.

Ntunga anashtakiwa kwa kupokea hongo ya shilingi 320,000 kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022.

Akisoma hati ya Mashtaka, Mwendeaha Mashtaka wa TAKUKURU, Bi. Vailet Achimpota amesema, Mshtakiwa huyo kwa tarehe tofauti kati ya Juni 1, 2023 hadi Julai 30, 2023 alipokea hongo hiyo kutoka kwa wanakijiji 16 wa Kijiji cha Kagunga, Kata ya Kasekese.

Lengo ni ili awagawie mashamba katika maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Kalaba uliopo Wilaya ya Tanganyika.

Mshtakiwa amekiri kosa na Mahakama imemhukumu kulipa faini ya shilingi 500,000 au kifungo cha miaka mitatu jela.

Aidha, mshtakiwa amepelekwa gerezani baada ya kushindwa kulipa faini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news