Rais Dkt.Mwinyi:Tunajifunza mengi kutoka kwa Mzee Malecela

DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema,viongozi na Watanzania wanajifunza mengi kutokana na historia ya utendaji kazi wa Mzee John Samwel Malecela.
Ni katika nyadhifa mbalimbali alizoshika serikalini na Chama Cha Mapinduzi na ataendelea kuwa hazina muhimu ya maarifa na uzalendo hapa nchini.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Aprili 21,2024 katika sherehe za Kumbukizi ya miaka 90 ya kuzaliwa Mhe.Mzee John Samwel Malecela, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika nyumbani kwake Uzunguni jijini Dodoma.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Mzee John Samwel Malecela kwa kutimiza umri huo na amemuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia umri mrefu na afya njema.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, Watanzania wataendelea kufaidika na busara, hekima, na ushauri wake katika kuiletea maendeleo nchi yetu na uzoefu wake mkubwa alionao Mzee Malecela katika uongozi, siasa na diplomasia ya Kimataifa.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi na dini wamehudhuria akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Cleopa Msuya, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye,
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Comrade Abdulrahman Kinana, Spika wa Bunge mstaafu Mhe.Job Ndugai, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule, Mwenyekiti wa UWT Taifa,Mary Chatanda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news