Wazawa ni kipaumbele katika miradi mbalimbali nchini-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo unazingatia dhana ya ushirikishwaji wa wahandisi wazawa kupitia miradi endelevu ya kimkakati ya uwekezaji nchini.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo Aprili 20, 2024 alipozindua Taasisi ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Zanzibar na Mkutano mkuu wa mwaka huu katika ukumbi wa Hoteli ya Verde, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali zote mbili ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinafanya jitihada ikiwemo kuweka mazingira wezeshi kujiajiri, kuhamasisha utambuzi wa fursa mbalimbali, kurejesha stadi za ujuzi, elimu ya uanagenzi vyuoni pamoja na kutenga bajeti kwa ajili utafiti na ubunifu mbalimbali.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali kwa upande wake kupitia Uchumi wa Buluu imeendeleza sera ya kuajiri wasanifu, wahandisi na wakadiriaji wazalendo.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali inathamini mchango wa fani mbalimbali katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ikiwemo miradi ya ujenzi.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewapongeza wakandarasi na washauri wazawa kwa kufanya kazi za uhandisi kwa ufanisi katika miradi mbalimbali waliyotekeleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news