Rais wa Comoro afika Zanzibar kutoa salamu za pole kwa Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutokana na kifo cha Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa Rais wa Visiwa vya Comoro, Azali Assoumani.
Viongozi hao walikutana Aprili 21,2024 huko Bweleo, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mzee Mwinyi alifariki dunia tarehe 29 Februari, 22024 jijini Dar es Salaam na kuzikwa tarehe 2 Machi 2024 kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais Dkt.Mwinyi amemshukuru Rais Assoumani kwa salamu za mkono wa pole na kuja kuwafariji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news