Rais Dkt.Samia ametutendea haki Tabora Kaskazini-Mbunge Maige

DODOMA-Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini-Uyui mkoani Tabora, Mheshimiwa Almas Athumani Maige amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha miradi mingi ya maendeleo jimboni humo kwa ustawi bora wa wananchi.
Ametoa pongezi hizo juzi wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 bungeni jijini Dodoma.

"Kwanza nianze na shukurani, Mheshimiwa Spika, Jimbo la Tabora Kaskazini, Mama Samia Suluhu Hassan kalitendea haki sana, kwa hiyo ninamshukuru sana na tunampongeza sana."

Mheshimiwa Maige amesema, ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika jimbo hilo miradi ya maendeleo ni mingi.

"Tumejenga majengo ya halmashauri ambayo hayakuwepo na ukumbi wa mikutano, lakini pia tumejenga hospitali ya wilaya.

"Lakini, vile vile tumejenga vituo vya afya vitatu, tumejenga shule mbili za sekondari, tumejenga shule moja mpya ya msingi, lakini vile vile tumekarabati madarasa, lakini pia tuna maji ya Ziwa Victoria vijiji 58 vya Tabora Kaskazini.

"Tuna umeme vijiji vyote vya Tabora Kaskazini, tumejengewa barabara, tunajenga kituo cha VETA na bado tunapata elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita.

"Mheshimiwa Spika, mambo haya si madogo kwa jimbo moja ambalo limepata jumla ya shilingi bilioni 55.6 katika kipindi cha miaka mitatu.

"Tunamshukuru sana Mama Samia, tunampongeza sana Mama Samia tumeona kwamba Mama huyu ni mwenye utu, upendo na ulezi kwa jimbo letu la Tabora Kaskazini,"amefafanua Mheshimiwa Maige.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news