Wakamatwa wakitorosha mifugo 514 kwenda nchi jirani

NA ABEL PAUL
TanPol

JESHI la Polisi Kikosi cha Kuzuia wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakitorosha mifugo 514 kwenda nchi jirani huku wakitumia vibali vya kampuni isiyohusika na mifugo hiyo.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP Simon Pasua amesema,kikosi hicho kwa kushirikina na wananchi Aprili 6,2024 katika Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha waliwakamata watu wawili wakiwa na mifugo 514 ambayo walikuwa wakiitorosha kwenda nchi jirani.
Kamanda Pasua amebainsha kuwa, watuhumiwa hao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na utoroshaji na kukiuka taratibu za uuzaji wa mifugo hapa nchini.

SACP Pasua amesisitiza na kuwataka wananchi kufuata taratibu za uuzaji wa mifugo ili kutokukumbana na mkono wa sheria na kulikosesha mapato Taifa huku akisema jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote watakaokiuka taratibu.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa mnada huo wa mpakani Namanga wamewaomba wananchi wenzao kufuata taratibu zilizopo ili kutokukumbana na mkono wa sheria pindi wanapotaka kusafirisha mifugo yao nje ya nchi.

Daktari wa Mifugo Mnada wa Mpakani Namanga Longido mkoani Arusha amewataka wafanya biashara kufuata taratibu huku akiwaomba wafanya biashara hao kufika na vibali vilivyo kamilika ili kuondoa usumbufu na wasimamizi wa Mnada huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news