Rais Dkt.Samia ateua na kutengua uteuzi

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Catherine Michael Mashalla.
Mbali na hayo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Jaji Winfrida Beatrice Korosso kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT).

Jaji Korosso ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na amemteua Bibiana Jospeh Kileo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, kabla ya uteuzi huu Kileo alikuwa Mkuu wa Mashtaka Mkoa (RPO), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mwanza.

Aidha, Mheshimiwa Rais amemteua Alice Edward Mtulo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huu Mtulo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Kesi na Udhibiti Ubora, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news