Sikukuu ya Eid wiki ijayo

ZANZIBAR-Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar inapenda kuwataarifu Wasislamu na Wananchi wote kuwa Sikukuu ya Eid itakuwa tarehe 10.04.2024 au 11.04.2024 kutokana na kutegemea kuamndama kwa Mwezi.

Sala ya Eid itasaliwa katika Msikiti wa Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini saa 1:20 asubuhi In shaa Allah

Aidha, Baraza la Eid litafanyika katika Ukumbi wa Polisi Ziwani saa 3 asubuhi kwa wale waliopata mialiko, Wananchi wengine wanaombwa kufuatilia shughuli hio kupitia vyombo vya mbali mbali vya habari.

Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika shughuli hiyo.

Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar inawatakiwa Waislamu na Wananchi wote kwa ujumla maandalizi mema ya Sikukuu hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news