Taarifa ya huduma ya maji Dar es Salaam na Pwani

DAR ES SALAAM (Aprili 1,2024)-Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inapenda kuwataarifu Wananchi na wateja wake kuwa huduma katika mitambo ya uzalishaji Maji katika mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini imerejea baada ya kukamilika kwa maboresho ya Umeme yaliyotangazwa hapo awali na TANESCO.
Huduma inaendelea kuimarika kwa kasi katika baadhi ya maeneo ya kihuduma DAWASA na mafundi wetu watakuwepo mitaani kuhakikisha changamoto za kihuduma zinatatuliwa kwa haraka.

Mamlaka inawashukuru Wananchi kwa uvumilivu na utulivu wakati wote changamoto hii.

Endelea kuwasiliana nasi kupitia huduma kwa wateja

0800110064(Bure)
0735 202021(Whatsap tu)

Imetolewa na
Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASA

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news