TANROADS kazini Gongolamboto jijini Dar es Salaam

DAR ES SALAAM-Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imehakikisha utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka kupitia Barabara ya Nyerere hadi Gongo la mboto unaendelea huku barabara ya kawaida ikiendelea kupitika hata katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini.
Akizungumza wakati alipofanya ziara katika mradi huo Meneja wa Miradi ya Mabasi yaendayo Haraka (BRT-3) iliyopo chini ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Frank Mbilinyi amesema, amefanya ukaguzi wa kawaida kumuhimiza mkandarasi kuhakikisha pamoja na athari za mvua, lakini barabara inapitika wakati wote.
“Tumeendelea kumuhimiza mkandarasi kuhakikisha maeneo yote yanayotekelezwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyerere - Gongolamboto yanapitika kiurahisi pamoja na athari za mvua kila baada ya mvua kukatika ahakikishe anaziba mashimo na kusawazisha ili kuwezesha kurejesha mawasiliano ya barabara japo kuna ujenzi unaendelea.

“Tunashirikiana vizuri na mkandarasi kuhakikisha anapokea maelekezo pale anapokuwa amerudi nyuma tunakumbusha pamoja mhandisi elekezi ili kuhakikisha kazi inafanyika vyema.”
Aidha,amewasa madereva wa magari kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu za uendeshaji barabarani ili kuondoa changamoto wakati huu wa mvua kubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news