Tanzania,Denmark zakubaliana

DAR ES SALAAM-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) amekutana na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark, Mhe. Dan Jørgensen ambapo nchi hizi mbili zimeangazia maeneo ya ushirikiano na kukubaliana kuongeza ushirikiano kwenye sekta za kimaendeleo.
Tanzania na Denmark zinaenda kuongeza ushirikiano kwenye maeneo ya biashara, miundombinu, umeme, uwekezaji, kubadilishana uzoefu kwenye teknolojia pamoja na nishati safi na salama ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira na tabianchi kwa manufaa ya jamii ya sasa na baadaye.
Pande zote mbili zimeonesha kufurahishwa na mwelekeo wa ushirikiano huu ambapo Denmark ilionesha dhamira hiyo kwa vitendo mwaka 2023 baada kutengua uamuzi wake wa kuufunga ubalozi wake nchini.
Waziri Jørgensen yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili inayotarajiwa kufikia tamati hapo kesho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news