VIDEO:Mheshimiwa Maige ampa kongole Rais Dkt.Samia, Biteko kwa matokeo chanya Wizara ya Nishati

DODOMA-Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini-Uyui mkoani Tabora,Mheshimiwa Almas Athumani Maige amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha fedha nyingi Wizara ya Nishati, hivyo kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2024/2025 bungeni jijini Dodoma.

"Nianze na kumshukuru Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipa wizara hii fedha nyingi za miradi ambayo imetekeleza.

"Mimi ninasema huyu ndiye Rais mwenye upendo kwa Watanzania wote, mwenye utu na ulezi wa wananchi wake, tumpongeze sana.

"Lakini, ninaomba nimpongeze pia Dkt.Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa usimamizi wake mzuri wa wizara hii mpaka ikafanya mambo makubwa;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news