Wakulima Kilolo watakiwa kuongeza matumizi ya mbolea

IRINGA-Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo amewataka wakulima wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuzingatia kanuni bora za kilimo na ushauri wa wataalamu unaolenga kuwasaidia na kuwawezesha kuongeza tija kwenye kilimo chao.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo akiwasili katika kituo cha mafunzo kwa wakulima cha Ilula Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa tarehe 21 Aprili, 2024. Ziara hiyo ya kikazi imelenga kuwafikia wadau ambao ni watendaji wa serikali, wafanyabiashara na wakulima ili kujadili na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo kwenye utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayohusu tasnia ya mbolea.
Ametoa wito huo leo tarehe 21Oktoba, 2024 alipotembelea kituo cha Mafunzo cha kampuni ya mbolea ya Yara na wakulima wa kijiji cha Ruaha Mbuyuni katika Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa kwa ziara ya Bodi na Menejimenti ya TFRA yenye lengo la kusikiliza changamoto za wadau wa tasnia ua mbolea na kuzitatua.

Akizungumza na wakulima wa maeneo hayo Dkt. Diallo amewataka kuongeza matumizi ya mbolea katika shughuli zao za kilimo kutakakopelekea kuongeza uzalishaji na kuinuka kiuchumi ukilinganisha na hali zao kiuchumi kwa sasa.

Aidha, ameeleza kuridhishwa na uwepo wa kituo cha mafunzo katika mji wa Ilula na kueleza kitasaidia katika kuhamasisha na kutoa elimu ya kilimo bora kwa wananchi na elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ikiwemo.

Naye Mkurugenzi wa TFRA, Joel Laurent, ametambua mchango wa kampuni ya Yara na kuipongeza kwa juhudi kubwa ya kuelimisha wananchi wa Kilolo juu ya kilimo bora na kubainisha kinasaidia kukuza tasnia ya mbolea.

Amepongeza programu ya kuhamasisha watoto kushiriki kwenye kilimo na kueleza elimu hiyo inawajengea hali ya kupenda shughuli za kilimo hata watakapokuwa watu wazima.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo (katikati) akiwa katika picha na watendaji wa serikali, wasimamizi wa kituo cha mafunzo na wakulima waliofika kwa kikao wakati wa ziara ya Bodi na Menejimenti ya TFRA kwenye kituo hicho tarehe 21 Aprili, 2024 Ilula- Kilolo mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo (katikati) akiwa katika picha na watendaji wa serikali, wasimamizi wa kituo cha mafunzo na wakulima waliofika kwa kikao wakati wa ziara ya Bodi na Menejimenti ya TFRA kwenye kituo hicho tarehe 21 Aprili, 2024 Ilula- Kilolo mkoani Iringa.
Leonard Nyabanga Meneja wa Kituo cha Mafunzo kwa wakulima kinachomilikiwa na kampuni ya mbolea ya Yara kilichopo kijiji cha Ilula Kilolo mkoani Iringa akieleza jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi na Menejimenti ya TFRA waliotembelea Kituo hicho kwa ziara ya kikazi iliyolenga kujifunza, kusikiliza na kutatua changamoto za wadau wa tasnia ya mbolea nchini.

"Programu kama hizi zinawaandaa watoto wetu kujua thamani ya kilimo kwenye maisha yao,"Laurent aliongeza.

Aidha, ameeleza matamanio yake kuwa ni kuona wananchi wengi wakiongezeka kwenye mnyororo wa thamani/ biashara ya mbolea na kuongeza matumizi ya mbolea Ili kufikia Agenda 10/30: Kilimo ni Biashara.

Kwa upande wake, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Kilolo,Tumsifu Charles alitoa shukrani zake kwa kampuni ya mbolea ya Yara Tanzania Ltd kwa kuchukua sampuli za udongo katika vijiji 16 walikoanzisha mashamba darasa kwa ajili ya wakulima kujifunza.

Pia, aliomba matokeo ya vipimo hivyo kurudishwa ili wakulima wanufaike kwa kutambua aina ya mbolea wanayotakiwa kutumia katika mashamba yao ilinkuondokana na kutumia mbolea kwa mazoea pasipo kupima afya ya udongo.

Ameeleza mpango wa ofisi yake wa kuanzisha programmu ya upimaji wa afya ya udongo katika kata na vijiji wanavyovisimamia kufuatia kupewa vifaa maalum kwa kazi hiyo kutoka Wizara ya kilimo na wadau wengine wa kilimo ambapo kwa sasa wanavifaa sita kwa kazi hiyo.

Naye, Donath Fungu Meneja wa Kilimo kwa Tanzaniq na Rwanda ameeleza kuwa kampuni yake hutoa mafunzo ya awali kwa wakulima kabla ya msimu ili kuwajengea uwezo wakati msimu wa kilimo unapowadia.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA,Dkt. Anthony Diallo akizungumza na wadau wa mbolea katika kikao kilichowakutanisha watendaji, wasimamizi wa kituo cha mafunzo kwa wakulima na wakulima wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa (hawapo pichani) tarehe 21 Aprili, 2024 ili kujifunza, kusikiliza na kutatua changamoto za wadau wa tasnia ya mbolea.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent, akizungumza na wakulima na wasimamizi wa kituo cha mafunzo wakati wa ziara ya Bodi na Menejimenti ya TFRA iliyolenga kujifunza, kusikiliza na kutatua changamoto za wadau wa tasnia ya mbolea nchini tarehe 21 Aprili, 2024 Kilolo mkoani Iringa.
Wakulima wa Ilula, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA,Dkt. Anthony Diallo (Hayupo pichani) akizungumza nao katika kikao kilichowakutanisha watendaji, wasimamizi wa kituo cha mafunzo kwa wakulima na wakulima tarehe 21 Aprili, 2024 ili kujifunza, kusikiliza na kutatua changamoto zao.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo akizungumza na wakulima wa kijiji cha Ruaha Mbuyuni Wilaya ya Kilolo alipokuwa katika ziara ya kujifunza kusikiliza na kutatua chanamoto za wadau wa mbolea mkoani Iringa tarehe 21 Aprili, 2024.

Amebainisha mpango wa kampuni wa kuajiri mtaalam wa kilimo kuanzia mwezi Mei, 2024 atakayehudumia wananchi watakaokua wakitembelea kituo cha mafunzo na kupewa huduma ya ushauri kwa muda wote wa kazi kuanzia saa 1.30 hadi saa 11 jioni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news