Wazabuni hatiani kwa rushwa Biharamulo

KAGERA-Mahakama ya Wilaya Biharamulo mkoani Kagera imewatia hatiani wazabuni wawili ambao ni Salanga Mayenga na Vedasto Kiporoka.
Washtakiwa wametiwa hatiani na kuamriwa walipe faini ya shilingi milioni moja au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la hongo.

Kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya washtakiwa Salanga Mayenga na Vedasto Kiporoka katika Shauri Namba 5943/2024, imetolewa Aprili 9,2024 na Mhe. Flora Ndare Hakimu Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo.

Ilidaiwa kwamba kati ya mwezi Mei na Juni 2023, washtakiwa walijipatia manufaa isivyo stahili ya hongo ya shilingi 3,278,700 katika manunuzi ya vifaa vya umeme.

Ni kwa kuzidisha malipo ya bei ya vifaa kwenye mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Kikomakoma mpya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo.

Aidha,washtakiwa wamelipa faini na kuachiwa huru na Mahakama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news