Waziri Aweso asisitiza utekelezaji agizo la Rais Dkt.Samia kwa mamlaka za maji nchini

*Ahimiza ufungaji wa mita za malipo ya kabla

DAR ES SALAAM-Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesisitiza Mamlaka za Maji Nchini ikiwemo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha agizo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la kufunga mita za malipo ya kabla kwa wateja kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi wote.
Ametoa wito huo wakati wa hafla ya futari ya DAWASA na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, Viongozi wa Mkoa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wadau wengine wa Sekta ya Maji iliyoenda sambamba na dua maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa ili kufanikisha utekelezaji wa agizo hilo, Wizara itashirikiana na Mamlaka za Maji Nchini kuhakikisha utekelezaji wa agizo hili unafanyika vizuri.

Mbali na hapo Mhe. Aweso ameitaka DAWASA kuongeza nguvu katika kukabiliana na upotevu wa maji kwenye maeneo yote ya huduma ili kuimarisha usambazaji wa maji kwa wateja wote.
Ameipongeza, mamlaka kwa kuendelea na utekelezaji mzuri wa majukumu yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi na kuahidi Wizara kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa ili huduma ya majisafi iweze kuwafikia wote sambamba na malengo ya Serikali ya kusambaza maji mijini kwa asilimia 95 na vijijini kwa asilimia 85 kufikia mwaka 2025.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala ndugu Edward Mpogolo ameipongeza Serikali kwa jitihada kubwa zinazofanyika za kuhakikisha huduma ya maji inafika kwa kila mwananchi.
"Kazi kubwa imefanyika na Serikali kwa kupitia DAWASA ya kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wote hususani wa Mkoa wa Dar es Salaam," ameeleza mdugu Mpogolo.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Ndugu Laston Msongole ameishukuru Wizara kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa DAWASA na kuwezesha utekelezaji mzuri wa majukumu ya kutoa huduma ya maji kwa wote.
Amesema,DAWASA imejipanga kikamilifu kuhakikisha utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la ufungaji wa mita za malipo kabla linatekelezwa na tayari zoezi limeanza kwa majaribio kwenye baadhi ya maeneo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news