Waziri Mkuu kufanya ziara Mlimba, kutembelea maeneo yaliyokumbwa na mafuriko

MOROGORO-Mkuu wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro,Mheshimiwa Dustan Kyobya ametoa rai kwa wananchi wa Halmashauri ya Mlimba kujitokeza kumlaki Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye anatarajia kufanya ziara kujionea maeneo yaliyoathirika na mvua.
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Mhe. Dustan Kyobya akizungumza katika mkutano wa hadhara huko Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro.

Wito huo ameutoa katika mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Mlimba tarehe Aprili 2024 ambapo amewaomba wananchi kujitokeza mapema kwa wingi Aprili 16,2024.
"Waziri Mkuu atapata nafasi ya kuwapa pole wenzetu waliokumbwa na mafuriko ya mvua na tutapata wasaa wa kuwasilisha taarifa zetu."
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,Mhe. Dustan Kyobya akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Bi. Zahara Muhidini Michuzi kwenye mkutano wa hadhara huko Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro.Mkuu wa wilaya ya Kilombero Mhe. Dustan Kyobya akiteta jambo na Katibu Tawala wa wilaya ya Kilombero, Abraham Mwaikwila katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Halmashauri ya wilaya ya Mlimba mkoani Morogoro.

“Nishukuru Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia kuokoa watu kama mnavyofahamu kutokana na mafuriko ya hayo ya mvua, treni ya Udzungwa iliyokuwa na watu ilizuiwa kufika Mlimba, lakini jeshi letu la Tanzania lilisaidia kuwaokoa watu na hakukutokea madhara yoyote,” alisema Mkuu wa wilaya.
Watendaji wa Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakiongozwa na Mratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu SACF-Ivo Alfred Ombella katika Mkutano wa hadhara huko Mlimba Halmashauri ya Morogoro.

Aidha,Serikali ilisaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko ya mvua kupata chakula cha msaada ambacho kililetwa na helikopta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news