IMF yaridhishwa na ufanisi wa Tanzania utekelezaji wa ECF, fedha zinakuja tena

NA PETER HAULE
WF

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ili Tanzania iweze kupata fedha za awamu ya nne kupitia Programu ya Extended Credit Facility-(ECF), itakayowezesha kuendelea kuchachua na kuimarisha uchumi kupitia sekta za uzalishaji.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa saba kulia) na Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Harris Charalambos Tsangarides (wa saba kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), baada ya kumalizika kwa kikao cha ufunguzi wa majadiliano ya kufanya tathimini ili Tanzania iweze kupata fedha za awamu ya nne kupitia program ya Extended Credit Facility (ECF), itakayowezesha kuchachua na kuimarisha uchumi kupitia sekta za uzalishaji, na namna ya Tanzania kuweza kupata fedha kupitia dirisha la Shirika hilo la Resilient and Sustainable Trust (RST) ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kilichofanyika jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Dodoma).

Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma kimehusisha timu ya wataalamu kutoka IMF walioongozwa na Bw. Harris Charalambos Tsangarides waliokuja kufanya tathmini na pia kujadili namna ya kuiwezesha Tanzania kupata fedha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha lake la Resilient and Sustainable Trust (RST).

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania inashukuru kwa msaada wa kiasi cha dola za Marekani milioni 455.3 zilizotolewa kwa awamu tatu za kwanza kati ya dola bilioni 1.1 ili kutekeleza miradi inayosaidia kuchochea maendeleo ya wananchi, kukuza uchumi jumuishi na kuiwezesha nchi kuhimili misukosuko ya kiuchumi inayoikabili Dunia.

“Tunaendelea kufanya kazi na wenzetu wa IMF kupitia programu ya ECF na sasa wamekuja kwenye misheni ya kusaidia Tanzania kuweza kunufaika na dirisha la Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi, programu hiyo ni mwendelezo wa programu za Shirika hilo za kuimarisha uchumi wa nchi wanachama wa Shirika hilo baada ya athari za Uviko 19,"ameeleza Mhe. Dkt. Nchemba.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati akifungua kikao cha Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ili Tanzania iweze kupata fedha za awamu ya nne kupitia program ya Extended Credit Facility (ECF), itakayowezesha kuchachua na kuimarisha uchumi kupitia sekta za uzalishaji, na namna ya Tanzania kuweza kupata fedha kupitia dirisha la Shirika hilo la Resilient and Sustainable Trust (RST) ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kilichofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Nchemba ameihakikishia IMF kuwa Tanzania itaendelea kutumia fedha zilizotolewa kulingana na makubaliano yaliyopo na pia amewapongeza kwa uamuzi wa kutembelea vivutio kama Ngorongoro na amewaomba wakipata nafasi waweze kutembelea maeneo mengine kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro na Zanzibar.

Alisema kuwa baada ya majadiliano na timu hiyo ya wataalam wa IMF Tanzania itapata sifa ya kuingia kwenye programu hiyo ya kunufaika na Mfuko wa RST ambapo kwa sasa haina vigezo hivyo.

Dkt. Nchemba aliishukuru IMF kwa niaba ya Serikali kwa msaada wake na miongozo katika utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF) kwa kuwa wamefanya jitihada kubwa katika kuhakikisha Tanzania inakidhi vigezo vya kupata fedha kutoka ECF kwa ajili ya kusaidia bajeti na changamoto zinazotokea duniani.
Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Harris Charalambos Tsangarides, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) uliofunguliwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ambapo watafanya tathimini ili Tanzania iweze kupata fedha za awamu ya nne kupitia program ya Extended Credit Facility (ECF), itakayowezesha kuchachua na kuimarisha uchumi kupitia sekta za uzalishaji, na namna ya Tanzania kuweza kupata fedha kupitia dirisha la Shirika hilo la Resilient and Sustainable Trust (RST) ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kilichofanyika jijini Dodoma.

Alisema maeneo ambayo IMF imekuwa ikishirikiana na Tanzania yanaenda sambamba na ajenda ya Serikali ambayo inakusudia kutengeneza mazingira bora ya sekta ya uzalishaji ambayo kimsingi ni maeneo ambayo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayapa kipaumbele.

Mhe. Dkt. Nchemba alieleza kuwa maeneo hayo kwa muda mrefu yanatoa majawabu kwa matatizo yanayowakabili watanzania, yakiwemo matatizo ya ajira, kupunguza umasikini na kuwajengea uwezo watanzania kwa kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji.

Alisema kuwa Serikali ipo tayari kwa majadiliano, ambapo timu ya Wizara ya Fedha na taasisi zake itaanza katika majadiliano hayo na pia itaratibu majadiliano na Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia mazingira na wizara nyingine za kisekta.

Kwa upande wake Kiongozi wa Timu hiyo ya IMF Bw. Harris Charalambos Tsangarides, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutekeleza kwa umahili mpango wa ECF na kutimiza vigezo vilivyoweka katika mpango huo kwa wakati na kusaidia nchi kupata kiasi cha dola za Marekani 455.3.

Amesema majadiliano hayo ni mwendelezo wa mjadala uliofanyika katika Mikutano ya Majira ya Kipupwe yaliyofanyika jijini Washngton D.C, Marekani, ambapo Tanzania iliwasilisha maombi ya kutaka kunufaika na dirisha lake la Resilient and Sustainable Trust (RST) ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hivyo wamekuja ili kufanya tathimini kwa kujadiliana na wadau namna ya kutekeleza maombi hayo.
Ujumbe wa Tanzania na Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), wakiwa katika kikao cha ufunguzi wa majadiliano ya kufanya tathimini ili Tanzania iweze kupata fedha za awamu ya nne kupitia program ya Extended Credit Facility (ECF), itakayowezesha kuchachua na kuimarisha uchumi kupitia sekta za uzalishaji, na namna ya Tanzania kuweza kupata fedha kupitia dirisha la Shirika hilo la Resilient and Sustainable Trust (RST) ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango nchini, Bw. Lawrence Mafuru (kushoto), Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila (katikati), Kaimu Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja (kulia), wakifuatilia kwa umakini ufunguzi wa kikao cha Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ili Tanzania iweze kupata fedha za awamu ya nne kupitia program ya Extended Credit Facility (ECF), itakayowezesha kuchachua na kuimarisha uchumi kupitia sekta za uzalishaji, na namna ya Tanzania kuweza kupata fedha kupitia dirisha la Shirika hilo la Resilient and Sustainable Trust (RST) ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), wakiwa katika kikao cha ufunguzi wa majadiliano ya kufanya tathimini ili Tanzania iweze kupata fedha za awamu ya nne kupitia program ya Extended Credit Facility (ECF), itakayowezesha kuchachua na kuimarisha uchumi kupitia sekta za uzalishaji, na namna ya Tanzania kuweza kupata fedha kupitia dirisha la Shirika hilo la Resilient and Sustainable Trust (RST) ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kilichofanyika jijini Dodoma.

Alisema kuwa baada ya majadiliano hayo watawasilisha hoja kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo kwa ajili ya kupitia ma kujadili mapendekezo yatakayotolewa.

Hali kadhalika Bw. Tsangarides aliahidi kuendekleza ushirikiano wa karibu kati ya IMF na Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news