Rais Dkt.Mwinyi asisitiza umuhimu wa usafiri wa anga nchini

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi kupitia usafiri wa anga ambao ni kichochea kikuu cha ukuaji wa uchumi.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Kongamano la sita la usafiri wa anga Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Hoteli ya Verde Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 15 Mei 2024.
Aidha,Rais Dk.Mwinyi ameeleza hatua iliyofikiwa na SMZ katika ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga ya kutekeleza miradi kwa kukamilisha jengo la abiria uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Terminal 3.

Vile vile, kuanza ujenzi jengo jipya la abiria Terminal 2 litakalohudumia abiria zaidi 1,300,000 kwa mwaka, ujenzi na ukarabati wa ujenzi wa jengo la zamani la Terminal 1.
Pia, ujenzi wa jengo la biashara na ofisi katika jengo la tatu la abiria, jengo la kuhifadhi na kusafirisha hasa vyakula vinavyoharibika kwa haraka.

Ujenzi wa vituo vitatu vya huduma za mafuta ya ndege, ujenzi wa uwanja wa ndege na upanuzi wa kiwanja cha ndege Pemba na jengo jipya la abiria na uwanja wa ujenzi wa kiwanja cha Nungwi.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza washiriki wote wa kongamano hilo kujadili na kutoa mapendekezo kwa kubainisha fursa zitazoweza kutumika katika sekta ya usafiri wa anga kwa manufaa ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news