Walimu ni chachu ya mageuzi ya elimu-Prof.Nombo

TANGA-Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Serikali inawathamini Walimu hivyo itaendelea kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha wanatekeleza wajibu wako kikamilifu.
Prof. Nombo ametoa kauli hiyo Mei 14, 2024 wakati akizungumza na Walimu wa Shule ya Msingi Bombo jijini Tanga, akisema Ualimu ni taalamu muhimu sana katika kutoa maarifa bora kwa watoto wa Kitanzania.

Aidha, amewahimiza walimu kutumia vema fursa za mafunzo endelevu kazini (MEWAKA) na kuhakikisha wanatekeleza vizuri Mitaala iliyoboreshwa pamoja na kutambua na kukuza vipaji na Stadi za Mawasiliano.
Amewataka walimu kuendelea kujifunza kupitia vitabu na mafunzo yaliyo katika Mfumo wa Mafunzo wa TET huku akiwashukuru kwa kuendeleza mafunzo hapo shuleni.

Naye Mkurugenzi Idara ya Ubunifu na Mitaala katika Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Godson Lema amewasisitiza Walimu hao kusoma kwa makini kupitia miongozo mbalimbali ili kutekeleza Mtaala ulioboreshwa.
Akizungumza Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Mwalimu Denis Mushi amesema tangu wameanza kutekeleza Mtaala Mpya wamepata mrejesho chanya kuelekea mageuzi ya elimu.

#ElimuUjuziMwelekeoWetu
#TunaboreshaElimuyetu
#Kaziiendelee

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news