Magazeti leo Julai 8,2024

DAR-Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amesema,alikuwa na urafiki wa karibu na baba mzazi wa marehemu Yusuf Manji tangu akiwa Afisa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla hajawa waziri wala Rais na kwamba siku chache kabla ya kifo cha baba yake Manji alimuomba yeye Dkt.Kikwete amlee mwanaye Yusuf.
Mheshimiwa Dkt.Kikwete amesema hayo Julai 7,2024 kwenye dua maalum ya kumuombea marehemu Yusuf Manji iliyoandaliwa na watoto wake Mehbub na Ali katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
"Nilikuwa natengeneza gari kule Quality Plaza Pugu Road na ndipo tulipofahamiana na baba yake Manji, baadaye alihamia Marekani na urafiki wetu uliendelea hadi nilipokuwa Rais.Baba yake Yusuf Manji alipokaribia kufariki alinikabidhi Yusuf na kuniomba nimlee, nikamwambia nitamlea, kwa hiyo baada ya kufariki rafiki yangu, Yusuf alikuwa kama mwanangu,”amebainisha Dkt.Kikwete.
Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news