IRINGA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 7, 2024 ameendelea na ziara mkoani Iringa ambapo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iramba iliyopo katika kijiji cha Iramba, kata ya Itandula kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPz1r23FMJtv-6Wn1yMOlBAjpKV9AxTuz5NehmmvS3Sx5-RC_7v0D7XLc0fep8U7YQAyGaFzQtoYcnl8vVnz_ZEL3o1nz_CvJeqCkXPsaQprPOJyKd4fq1w_vIHMVewI1YMiN3F3JTYDeToq0Gc0l6MxwwwQhFS_uEYsXJrCB62nKUawVDoHOMQnwTkLM/s16000/IMG-20240707-WA0045.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBl7JSVTivv8KOSq0W2OFiZi7GD7zysX7yrEQmLe5aT682FDjIMJ8DJwMk9TwCYZP-vhgH8um6ai24tqQkIvKeizQ-2PmUXz_W2SSVQnsZb97BXb2oRHtSxK8joCdl6QrEaCI4fVuU9RZ1lvkLk-HKJHnthO6QVdV8KiNIh75HeqywaKNUcZ8D0s69h5E/s16000/IMG-20240707-WA0043.jpg)
Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewataka kutumia fedha iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ili miundombinu yote itakayojengwa iendane na fedha iliyotolewa.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa ameagiza kupitiwa kwa gharama za ujenzi wa nyumba za walimu kupitia kamati ya elimu ya halmashauri “Fanyeni mapitio ya fedha mliyopanga kutumia kwa ajili ya nyumba za walimu, shilingi milioni 100 ni nyingi kwa nyumba moja.”
Pia ameagiza kuondolewa na kurudishwa kwa fundi madawati yote ambayo hayana eneo la kuweka daftari kwa ajili ya wanafunzi.
Ujenzi wa Shule hiyo unategemewa kugharimu kiasi cha Bilioni 1.78 mpaka kukamilika kwake, ukihusisha jengo la utawala (1) Madarasa (8) Ofisi (4), Maabara (1), Chumba cha TEHAMA (1) Nyumba za walimu (5), Bwalo la chakula (1) na Mabweni (4).
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfJhg3vexiQtst0G1FtpMJSYPwguajlUcQ7t4h5SjsxQlxs0TuS0QU-8T1_j4zu4aQSTBjA876B1nhigipDHETq4vtBB0BoR75WlOFukgWG2ytqrsHKwcR1PJcLJ3b7FipYc9ONgxNPp9-bhRQrhFMvfilv_8N44Rdf57igvz_h_8tL3dzbzHcbSZ7a9M/s16000/IMG-20240707-WA0029.jpg)
Kwa sasa shule hiyo ina jumla ya madarasa 8, Ofisi 4 na bweni lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 lipo katika hatua ya kuwekwa marumaru.