Rais Dkt.Samia afanya uteuzi UTT-AMIS, IRDP na EASTC

MOROGORO-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

(i) Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS.

Prof.Kamuzora ni Katibu Tawala wa Mkoa Mstaafu,anachukua nafasi ya Bw.Casmir Kyuki ambaye amemaliza muda wake;

(ii) Prof. Joseph Andrew Kuzilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza laUongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP).

Prof. Kuzilwani Profesa Mstaafu, Chuo Kikuu
cha Mzumbe; na

(iii) Prof. Ahmed Mohamed Ame ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kwa
kipindi cha pili.Uteuzi huu umeanza Agosti 4,2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news