Rais Dkt.Mwinyi aendelea kuwaheshimisha wajasiriamali na wafanyabiashara nchini, afungua soko la kisasa Jumbi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameaziagiza taasisi zinazosimamia masoko mapya kuweka viwango vidogo vya malipo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili wamudu kulipa na kuendelea na biashara katika mazingira mazuri.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 27, 2024 alipofungua soko jipya la kisasa la Jumbi, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia Wafanyabiashara kuwa Serikali itaendelea kuwaandalia mazingira bora zaidi sokoni hapo yatakayoendana na soko hilo.
Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa, Serikali imetenga kiasi cha shillingi bilioni 100 kwa ajili ya kuwapatia mitaji wajasiriamali na wafanyabiashara kuimarisha biashara zao.

Ametoa rai kwa wajasiriamali ambao bado hawajapata mitaji kujipanga vema katika Vikundi ili Serikali iwapatie mitaji hiyo.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameruhusu wafanyabishara kufanya shughuli zao muda wote na kuagiza soko kuwa wazi Usiku na mchana.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amewaahidi wananchi kuwa ataendelea kujipambanua kwa Vitendo kutimiza ahadi alizoziahidi wakati wa Kampeni mwaka 2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news