IRINGA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani amesema Mfereji Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mkombozi unaojengwa na Serikali katika Bonde la Pwaga utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika kujishughulisha na kazi za kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Mfereji wa Mkombozi wakati wa ziara yake katika Tarafa ya Pwaga.
Waziri ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo na kufanya Mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Mbuyuni, Kimande, Itunundu, Mbugani, Mboliboli katika Jimbo la Isimani mkoani Iringa tarehe 30 Septemba,2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akipokea taarifa ya Maendeleo ya ujenzi wa Mfereji wa Mkombozi kutoka kwa Mhandisi Abdulhamid Mbaba alipotembelea eneo la ujenzi wa Mfereji lililopo tarafa ya Pwaga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akipokea taarifa ya Maendeleo ya ujenzi wa Mfereji wa Mkombozi kutoka kwa Mhandisi Abdulhamid Mbaba alipotembelea eneo la ujenzi wa Mfereji lililopo tarafa ya Pwaga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akiwa katika eneo la Mfereji ambao upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake kukamilika.
Uwekezaji unaofanya na Serikali utasaidia kuwainua wananchi wengi kiuchumi kwa kuwa na maisha bora zaidi kwa mashamba wanayolima lakini kwa mashamba mengine mapya hekari 15000.
“Tunamponge sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa wa uchumi wa Mkoa wa Iringa na kwa Bonde la Pawaga,” alisema Waziri Lukuvi.
Tunaamini Mkandarasi utautekeleza Mradi wa ujenzi kwa ufanisi mkubwa, na Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake kwa kuhakikisha fedha za mradi zinapatikana ili mradi huo wa umwagiliaji ulio mkubwa kuliko miradi mingine yeyote ya umwagiliaji ukamilike kwa wakati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani katika picha akiwa katika Mkutano wa Hadhara uliokutanisha vijiji viwili vya Mbugani na Mboliboli.
Kwa Upande wake Mhandisi wa Ujenzi wa Mfereji wa umwagiliaji Abdulhamid Mbaba kutoka Comfix and Engineering Limited amesema mradi bado upo kwenye hatua za utekelezaji kwa kuhusanisha ujenzi wa miundo mbalimbali kama Ujenzi wa Banio, Ujenzi wa Mfereji Mkuu, Ujenzi wa Barabara na Ujenzi wa Vigawa Maji kwa Lot namba 1.
Ujenzi wa Lot namba 2 unahusisha Ujenzi wa Mfereji Mkuu wenye Urefu wa Km 16.1, Ujenzi wa Tuta la kuzuia Mafuriko na Barabara na Ujenzi wa Vigawa Maji.
Mhandisi Mbaba amesema, “Ujenzi wa Lot namba 1 Ujenzi wa banio umekamilika kwa 98%, Ujenzi wa Mfereji Mkuu na Kichuja Mchanga umekamilika kwa 50% huku Ujenzi wa Barabara ukikamilika kwa 95%.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani katika picha akiwa katika Mkutano wa Hadhara uliokutanisha vijiji viwili vya Mbugani na Mboliboli.
Aidha kwa Lot namba 2 Ujenzi wa Mfereji Mkuu na Kichujio Mchanga umetekelezwa kwa 36% Ujenzi wa Kichujio Mchanga na barabara umefikia 62%.