DAR-Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo ameteuliwa na CAF kuwa Ofisa Habari wa mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya Young Africans Sports Club ya Tanzania na Al Hilal SC ya Sudan.
Mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Novemba 26,2024.