DAR-Klabu ya Yanga SC imemtangaza Miloud Hamdi mwenye uraia wa Algeria na Ufaransa kuwa kocha wake mpya akichukua mikoba ya Sead Ramovic ambaye anaondoka klabuni hapo baada ya kuvunja mkataba na kocha Mjerumani huyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Kocha huyo mbali na uzoefu alionao, pia ana mafanikio makubwa katika soka la Afrika akishinda taji la Ligi Kuu ya Algeria na kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu wa 2015-2016 akiwa na USM Alger.