Rais Dkt.Mwinyi afuturisha wananchi Mkoa wa Mjini Magharibi, asisitiza amani na mshikamano

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika kula futari ya pamoja aliyowaandalia.
Hafla hiyo imefanyika Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Akizungumza katika futari hiyo,Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi kuendelea kuiombea nchi amani pamoja na viongozi wakuu ili waendelee kuiongoza nchi kwa amani na waendelee kutekeleza mambo ya maendeleo.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar,Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation,Mama Mariam Mwinyi.
Rais Dkt.Mwinyi amekuwa na utaratibu huo kila mwaka unaofanyika katika mikoa yote ya Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news