DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ((Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya Ujezi wa Reli ya CRCC ya China, ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bw. Zhao DianLong, iliyotia nia ya kuwekeza kwenye Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba, aliiahidi Kampuni hiyo utayari wa Serikali wa kushirikiana nayo kuboresha miundombinu ya mradi huo wa kihistoria ili kukuza biashara na uchumi kati ya Tanzania na Zambia katika sekta ya usafirishaji.