Dkt.Kikwete awasilisha ujumbe wa Rais Samia kwa Rais Jenerali Abdourahamane Tchiani

NIAMEY-Rais Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo na Rais wa Niger, Mhe. Jenerali Abdourahamane Tchiani katika Ikulu ya Niamey April 16, 2025.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kikwete ambaye ni mwanadiplomasia nguli aliwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Jenerali Tchiani.
Aidha, katika mazungumzo hayo, Mhe. Kikwete aliwasilisha salamu za Rais Samia ambapo alielezea kufurahishwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Niger na kusisitiza umuhimu wa kukuza na kuuimarisha zaidi katika nyanja za biashara, uwekezaji na utalii.

Alisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kubadilishana uzoefu na ujuzi ili utajiri mkubwa wa maliasili uliopo uweze kuvunwa na kuendelezwa kwa faida ya wananchi wa bara hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news