DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania fedha zilizokusanywa katika mbio za hisani za Bunge zitakwenda kutumika kama ilivyokusudiwa.

Ujenzi wa shule hiyo shule hiyo itakayokuwa na uwezo wa kusajili wanafunzi wasiopungua 300 hadi 350 kwa mwaka utagharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu.
Shule hiyo ya kidato cha tano na sita itajengwa katika eneo la Kikombo jijini Dodoma karibu kidogo na shule ya wasichana iliyojengwa na wabunge wanawake 2020.
“Ninawapongeza sana Wabunge wenzangu kwa kuweka alama na kugusa maisha ya Watanzania na watoto wetu wa kiume watakaopata fursa ya kusoma katika shule hiyo.”
Amesema ujenzi wa shule hiyo ni mpango wa Bunge wa kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza na kuendeleza sekta ya elimu.

Shule hiyo ya bweni itakuwa na maabara nne za biolojia, kemia, fizikia na jiografia, maktaba, bwalo la chakula, nyumba za walimu pamoja na viwanja vya michezo.

Awali, Mwenyekiti wa Mbio za Hisani za Bunge, Festo Sanga alisema lengo la mbio hizo ni kukusanya fedha za ujenzi wa shule ya wavulana. Mbio hizo zilihusisha watu zaidi ya 4,000.