WASHINGTON D.C-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, pamoja na Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, wanashiriki Mikutano ya Msimu wa Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.
Mikutano hiyo ya mwaka 2025 imebeba kaulimbiu isemayo “Ajira: Njia ya Mafanikio”, na inatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 21 hadi 26 Aprili 2025.
Gavana Tutuba na Naibu Gavana Kayandabila ni miongoni mwa ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ambaye pia ni Gavana wa Benki ya Dunia kwa upande wa Tanzania.
Mikutano hii inatoa fursa kwa viongozi wa nchi wanachama wa IMF na Benki ya Dunia kujadili maendeleo ya kiuchumi duniani, changamoto zinazokabili mataifa mbalimbali, na fursa za ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya ustawi wa jamii.