DAR-Mkuu wa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Furahika kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam,Dkt.David Msuya ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Buguruni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa CCM Kata ya Buguruni,Saida A.Yamba uteuzi huo ulifanyika Machi 18,2025 katika kikao maalumu cha Kamati ya Siasa ya Halmashauri ya Kata.
Aidha,Dkt.Msuya baada ya uteuzi huo anatarajiwa kuhudhuria kikao cha pamoja cha Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Kata kitakachofanyika Aprili 22,2025 katika ofisi za kata saa 10 jioni.
