LONDON-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshuhudia kusainiwa kwa hati mbalimbali za makubaliano baina ya wizara na taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Commonwealth Enterprise and Investment Council (CWEIC), Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA) na Taasisi ya Geopatners Ltd ya Uingereza, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Nutri-San Limited (UK), The Scottish Association for Marine Science (UK) pamoja na Chuo cha Kilimo cha Royal (UK) katika ukumbi wa Guildhall Art Gallery jijini London leo Aprili 9,2025.
Hati hizo za makubaliano zilizosainiwa zitaisaidia kuleta ufanisi zaidi sekta mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Buluu na Uwekezaji.

















