Rais Dkt.Mwinyi awatakia wananchi wote Pasaka njema,ahimiza amani na utulivu
ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewatakia Wakristo na wananchi wote Sikukuu njema ya Pasaka huku akiwahimiza kusheherekea kwa amani na utulivu.