Rais Dkt.Samia awasili mjini Luanda

LUANDA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Luanda, Jamhuri ya Angola kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu kuanzia leo tarehe 7 hadi 9 Aprili 2025. Ziara hii inafanyika kufuatia mwaliko rasmi wa Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe.João Manuel Gonçalves Lourenço.  Lengo kuu la ziara hii ni kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kimkakati kati ya Tanzania na Angola.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 de Fevereiro, Rais Samia amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe.Tete António akiambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.

Viongozi wengine waliokuwapo ni Balozi wa Tanzania nchini Angola mwenye Makazi yake nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro de Oliveira pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Ziara hii ni ya kihistoria, kwani ni mara ya kwanza kwa Rais wa Tanzania kutembelea Angola katika kipindi cha miaka 19, tangu ziara ya mwisho ya Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa madarakani mwaka 2006.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news