ZANZIBAR-Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amekabidhi Shilingi Milioni 20 ya goli la mama kwa Simba SC baada kufanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Stellenbosch katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika mchezo ulifanyika katika uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.