ZANZIBAR-Jean Charles Ahoua dakika ya 45' ameiwezesha Simba Sports Club kujikusanyia alama tatu za muhimu katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi huo umewesha matokeo ya 1-0.
Ni katika mtanange uliowakutanisha na Stellenbosch ya Afrika Kusini leo Aprili 20,2025 katika Dimba la Amaan Complex jijini Zanzibar.
Leo Kocha Mkuu, Fadlu Davids amepanga kikosi kile kile kilichocheza mechi mbili za robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Al Masry.
Aidha, Simba SC ilikosa fursa kadhaa za ushindi mnono kupitia kikosi kilichoundwa na Moussa Camara (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Karaboue Chamou (2), Abdurazak Hamza (14), Yusuph Kagoma (21),
Wengine ni Kibu Denis (38), Fabrice Ngoma (6), Steve Mukwala (11), Jean Charles Ahoua (10), Elie Mpanzu (34).
Wachezaji wa akiba walikuwa ni Ally Salim (1), David Kameta (3), Valentine Nouma (29), Augustine Okejepha (25), Edwin Balua (37), Debora Fernandes (17), Awesu Awesu (23), Leonel Ateba (13), Joshua Mutale (26).
Simba SC na Stellenbosch wanatarajia kurudiana Aprili 27,2025 kwenye Dimba la Moses Mabhida mjini Durban, Afrika Kusini.
Aidha, mshindi kati ya Simba na Stellenbosch atakutana na mshindi wa mechi kati ya RS Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria katika fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.