Uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa asilimia zaidi ya saba-Rais Dkt.Mwinyi

LONDON-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema katika kipindi cha Miaka 4 Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua kwa kasi zaidi ya asilimia 7 kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta mbalimbali.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika kwenye chakula cha jioni na Viongozi mbalimbali wa Wafanyabiashara wa Uingereza kilichoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) katika ukumbi wa Serikali ya Uingereza Jijini la London, tarehe 8 Aprili 2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewakaribisha Wawekezaji kutoka Uingereza kuwekeza Zanzibar katika fursa mbalimbali ikiwemo sekta ya Uchumi wa buluu, utalii, usafiri wa baharini, uvuvi, nishati na miundombinu ya kidijitali.

Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Uingereza wamehudhuria hafla hiyo akiwemo Alderman Professor Emma Edhen, Alderman City of London na Lord Malhard, House of Lords, na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Commonwealth, Lord Darroch wa House of Lords.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news