Rais Dkt.Mwinyi afanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza

LONDON-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuunga mkono juhudi za Zanzibar katika kuboresha miundombinu ambapo hivi karibuni Taasisi ya UK Export Finance ya Uingereza imetoa dhamana kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pemba pamoja na miundombinu ya barabara Unguja na Pemba.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza,Mhe.Angela Rayner tarehe 8 Aprili 2025 jijini London.
Naye, Mhe.Rayner ameeleza kuwa Serikali ya Uingereza imeweka kipaumbele cha kukuza uchumi ambapo kupitia mahusiano na mataifa rafiki itakuwa tayari kukuza biashara na uwekezaji Zanzibar.

Halikadhalika, Tanzania na Uingereza zakubaliana kukuza zaidi ushirikiano katika biashara na uwekezaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Mutual Prosperity Partnership, makubaliano hayo yamefikiwa tarehe 8 Aprili 2025 wakati wa mazungumzo baina ya Rais Dkt.Mwinyi na Naibu Waziri Mkuu huyo jijini London.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news