Waziri Mkuu aridhishwa na maandalizi kuelekea Sherehe za Mei Mosi

SHINYANGA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na Maandalizi kuelekea sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei Mosi, 2025 kitaifa Mkoani Singida katika Uwanja wa Bombadia.Ameyasema hayo leo Aprili 30, 2025 alipopokea taarifa na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe hizo. Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kamati inayoratibu sherehe hizo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha maeneo machache yaliyobaki ambayo yanahitaji maboresho.
Awali, akitoa taarifa ya maandalizi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa na wapo tayari kumpokea Rais Dkt. Samia kwa ajili ya sherehe hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news