BAKWATA yatangaza tarehe ya Sikukuu ya Eid El-Adh’ha kwa mwaka 2025

DAR-Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Adh’ha kwa mwaka 2025 itafanyika Jumamosi ya Juni 7,mwaka huu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 29,2025 na Katibu Mkuu BAKWATA, Alhaj Nuhu Mruma, kwa Waislamu na wananchi wote nchini, ikibainisha kuwa maandalizi ya sherehe hiyo yanaendelea kufanyika kwa ustadi.

Kwa mwaka huu, BAKWATA imetangaza kuwa sherehe za kitaifa za Eid El-Adh’ha zitafanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Sala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, uliopo Makao Makuu ya BAKWATA Kinondoni kuanzia saa 1:30 asubuhi. Baada ya swala, Baraza la Eid litaendelea katika eneo hilo hilo.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania,Dkt.Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana ametumia nafasi hiyo kuwatakia Waislamu na Watanzania wote maandalizi mema ya kusherehekea Sikukuu hiyo kwa amani, mshikamano na kumcha Mwenyezi Mungu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news