Balozi CP Hamad afanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda nchini Msumbiji

MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anawakilisha Madagascar na Ufalme wa Eswatini, Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad leo Mei 28,2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Kanali mstaafu Donat Ndamage, Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini Msumbiji.
Mkutano huo ni sehemu ya zoezi la kujitambulisha rasmi katika Jumuiya ya Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini Msumbiji. Katika mazungumzo yao pia walisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa ukaribu kwa maslahi ya Serikali na Wananchi wa nchi hizi mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news