BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeshiriki katika Soko la jumla la Fedha za Kigeni (IFEM) kwa mujibu wa Sera yake ya ushiriki katika soko la Fedha za Kigeni ya mwaka 2023.

Katika ushiriki huu, Benki Kuu imeuza Dola za Marekani milioni 35 kupitia mnada wa ushindani kwa kiwango cha wastani cha kubadilisha fedha za kigeni cha Shillingi 2,697.17 kwa Dola moja ya Marekani.
Mnada ulifanyika kupitia mfumo wa kielekroniki wa kufanyia Minada ya Fedha za Kigeni yaani “FX Auction System”.
Mnada huu ulifanyika kwa dhumuni la kuongeza ukwasi katika Soko la Fedhaza Kigeni na kama sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Fedha ya Benki Kuu.
