DCEA yawajengea wananchi Tarime uelewa juu ya madhara ya dawa za kulevya

MARA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imetoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya kwa wananchi na wanafunzi katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Mamlaka kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Katika hatua hiyo, DCEA ilitoa elimu kwa wanafunzi takribani 1,700 na walimu 39 wa Shule za Sekondari Manga na Kibasuka.Sambamba na hilo, elimu hiyo ilitolewa kwa wananchi 300 wa vijiji vya Nyarwana na Weigita vilivyopo wilayani humo.
Hata hivyo, kutokana na kukithiri kwa kilimo cha bangi katika maeneo hayo, uongozi wa serikali za vijiji umeanzisha sheria ndogo za udhibiti wa dawa za kulevya, kwa lengo la kuhakikisha kilimo hicho kinaondolewa kabisa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news