DODOMA-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Mei 29,2025 ameshiriki Mkutano Maalum wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.



















