Dkt.Sidi Quld Tah ndiye rais mpya wa AfDB


Waziri wa Fedha wa Tanzania, ambaye pia ni Gavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Gavana Mbadala (alternating Governor) wa Benki hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakifuatilia matukio mbalimbali baada ya Bodi ya Magavana ya Benki hiyo kumchagua kwa kura nyingi, Dkt.Sidi Quld Tah (Raia wa Mauritania), kuwa Rais Mteule mpya wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), katika uchaguzi uliofanyika leo tarehe 29 Mei 2025, katika Hoteli ya Sofitel Ivoire, Jijini Abidjan nchini Côte D’ivoire, ambaye anachukua nafasi ya Rais wa Benki hiyo aliyemaliza muda wake, Dkt. Akinumwi Adesina.
Dkt. Tah, Waziri wa zamani wa Fedha wa Mauritania, ameshinda kwa wastani wa asilimia 76.18 ya kura zote zilizopigwa, raundi ya tatu ya mchuano huo.

Alikuwa akiwania nafasi hiyo na wagombea wengine wanne akiwemo Bw. Amadou Hott (Senegal), Samuel Maimbo (Zambia) Abbas Mahamat Tolli (Chad) na mwanamke pekee katika kinyang’anyiro hicho, Bi. Bajabulile Swazi Tshabalala kutoka Afrika Kusini.
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ilianzishwa mnamo mwaka 1964 na mwaka huu ikiwa imetimiza umri wa mtu mzima wa miaka 60, ikiwa na wanachama 81, zikiwemo nchi 54 za Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news